Trending News>>

Lionel Messi azitaja timu tishio kombe la dunia lakini ataja timu anayoihofia zaidi.


Pamoja na kuchelewa kufika lakini timu ya taifa ya Argentina ilifanikiwa kufudhu kwa fainali za kombe la dunia zitakazochezwa mwakani nchini Urusi na shukrani zimeuendee Lioneil Messi aliyewabeba katika mchezo wa mwisho.
Lakini wakati wakijiandaa kushiriki michuano hiyo ya kombe la dunia, mshambuliaji huyo hatari wa klabu ya Barcelona tayari kichwani ana orodha ya timu ambazo anaamini zitakuwa tishio kwenye michuano hiyo.
Messi anaamini timu ya taifa ya Ujerumani ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo ni kati ya timu anazozipa nafasi kubwa bila kusahau Ufaransa, Brazil na timu ya taifa ya Hispania.
Lakini Lioneil Messi pamoja na kuzikubali timu hizo lakini kuna timu moja anayoiogopa zaidi nayo ni timu ya taifa ya Hispania ambayo amekiri kwamba hatamani kabisa kukutana nao katika michuano hiyo.
Lioneil Messi anaamini kwa sasa timu ya taifa ya Hispania ndio timu bora na wanacheza vizuri sana hivyo itakuwa ngumu kupambana nao haswa katika michuano mikubwa kama kombe la dunia.
Kuhusu kufudhu katika michuano hiyo kwa tabu sana Messi amesema aliamini watakwenda Urusi hata kama itachukua muda na ndio maana siku ya mchezo aliwaambia wachezaji wenzake watulie wanaelekea Urusi.

No comments:

Powered by Blogger.