Kwamba Man City Wasifungike
MANCHESTER City walivyouanza msimu, wamesababisha watu waamini kuwa huu ni mwaka wao wa kumaliza ligi bila kufungwa mechi yoyote.
Wanafanya vizuri England. Wanafanya vizuri Ulaya. Wameshinda mechi 14 mfululizo za michuano yote. Tayari wameshatengeneza maswali kama kuna timu yoyote ambayo inaweza kuwafunga katika msimu huu wa Premier. “Kama maamuzi yatakuwa yanawabeba namna hiyo nyumbani, hawatasimamishwa,” anasema kocha Arsene Wenger, akitolea mfano wa kupewa bao la kuotea na penalti ya utata katika kipigo cha Arsenal cha mabao 3-1 kutoka kwa vijana hao wa Pep Guardiola.
Hata hivyo, kusema kwamba Manchester City haitafungika, bado ni nadharia ya mapema sana. Historia ya Premier i n a o n y e – s h a kuwa kuna wakati City itasimamishwa hasa z i k i f i k a nyakati ngumu. Kumbuka kwamba bado hawajakutana na wapinzani wao halisi wa ubingwa, Manchester United na Tottenham. City wana u i m a r a m k u b w a na upana katika kikosi, lakini h a w a n a mchezaji a m b a y e anaweza k u z i b a v y e m a
pengo la Fernandinho. Pia hakuna anayeweza kuvaa vizuri viatu vya Kevin de Bruyne. Kama wachezaji hao wakiumia, basi tutarajie lolote. Soka ambalo Man City wanacheza, linahitaji kila siku uwe katika ubora wa juu ili ushinde, ndiyo maana siku ambayo hawakuwa kwenye ubora, timu ya daraja la chini, Wolves, iliwabana kwa dakika 120, hadi ikaja kufungwa kwa mikwaju ya penalti. K u s e m a kwamba City itakuwa timu nyingine ambayo
haitafung i k a msimu m z i ma bado ni mapema sana. “Kuna timu itatufunga,” alisema Guardiola Ijumaa iliyopita. Timu ya Wenger ya msimu wa 2003-04 ni pekee ambayo imemaliza msimu wa Premier bila kufungwa mechi yoyote tangu 1889, hiyo pekee inaonyesha ugumu wa kufanya hivyo katika soka la England. Suala hili halipaswi kabisa kuanza kuzungumzwa kabla ya Januari.
Tottenham ilicheza mechi nyingi zaidi bila kufungwa mwanzoni mwa msimu uliopita, ni kama ilivyofanya Chelsea msimu wa 2014-15, hata City ilicheza mechi nyingi zaidi bila kufungwa msimu wa 2012-13, na Liverpool ilifanya hivyo msimu wa 200708. Moja tu kati ya timu hizo nne ilifanikiwa kubeba ubingwa. Kuna timu ambazo zilianza msimu zikiwa hazijafungwa mechi mara mbili zaidi ya zile ilizocheza Man City lakini zikamaliza msimu zikiwa zimefungwa mara nyingi tu: Manchester United haikupoteza mchezo wowote katika mechi
zake 24 za kwanza za ligi msimu wa 2010-11, Liverpool haikupoteza mechi 29 za kwanza msimu wa 198788 au Leeds haikupoteza mechi 29 za kwanza msimu wa 1973-74, ambapo mwisho walifungwa mechi nne.
Pia, kuna dhana nyingine inayoenea kwa kasi kwamba Man City haiwezi kukamatwa kwa sasa, eti kisa wanaongoza kwa tofauti ya pointi nane. Huo ni upotoshaji mkubwa, kumbuka miaka sita iliyopita, kikosi cha Manchester United ambacho kilikuwa kimeshinda ubingwa mara nne katika miaka mitano nyuma, kilikuwa kinaongoza kwa tofauti ya pointi nane zikiwa zimebaki mechi sita, lakini Man City ikawa bingwa.
Haishangazi kocha Jose Mourinho alivyosema Jumapili iliyopita kwamba: “Tofauti ya pointi nane England siyo sawa na tofauti ya pointi nane Ureno, La Liga na Bundesliga.” Hili siyo pengo lisilofikiwa England. Real Madrid haijawahi kutoka nyuma kwa tofauti ya pointi nane na kushinda ligi,
lakini Man United ilikuwa nyuma ya Newcastle kwa tofauti ya pointi 12 msimu wa 1995-96 na ikatwaa ubingwa. Misimu mitatu nyuma, Chelsea ya Mourinho ilikuwa mbele ya City kwa tofauti ya pointi nane, lakini vijana wa Manuel Pellegrini wakafanya kweli hadi wakalingana pointi, hata hivyo mwishowe Chelsea ikashinda ubingwa. Hata hivyo, pamoja na haya yote, hakuna ambaye anaweza kupuuza ubora wa City.
Imekuwa ni timu bora zaidi, timu imara zaidi na ya kuangaliwa zaidi hadi sasa, lakini kutamba katika baadhi ya vipande vya msimu, ni suala moja, na kumaliza msimu bila kufungwa ni suala jingine. Kumbuka kuwa hata msimu wa 2011-12, City ilikuwa na mwanzo kama huu, ilishinda mechi 10 kati ya 11, na ilikuwa na bao moja zaidi ya iliyofunga msimu huu lakini mwishowe ilipoteza mechi tano. Na ilibidi isubiri hadi bao la dakika ya 94 kwenye mechi ya mwisho kutwaa ubingwa kwa tofauti ya magoli.
LONDON, ENGLAND Makala – Ulaya
No comments:
Post a Comment