Trending News>>

Bayern Kutafuta Pointi Muhimu Bundesliga


BUNDESLIGA itaendelea tena wikiendi ijayo wakati Bayern Munich watakapokuwa uwanjani kutafuta ushindi muhimu kwenye ligi hiyo kubwa. Bundesliga ni ligi mashuhuri kwa sasa na kwa Tanzania imekuwa ikionyeshwa moja kwa moja na King’amuzi cha StarTimes ambacho ni bora zaidi hapa nchini. Katika michezo hiyo ya Bundesliga, Bayern ambao wapo k i l e l e n i kwenye ligi
hiyo watakuwa wakipambana kwa nguvu kubwa kupata pointi tatu kwenye mchezo mgumu dhidi ya Augsburg. Hii ni kati ya timu ngumu kwenye Bundesliga na Bayern watatakiwa kuhakikisha wanaonyesha kiwango cha juu sana kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi.

Hawa wapo nafasi ya kumi kwa sasa wakiwa na pointi 16, kumi nyuma ya Bayern walipo kileleni lakini wamekuwa wakionyesha kiwango cha juu kwenye kila mchezo. Mchezo mwingine wa Jumamosi ni kati ya Hoff enheim dhidi ya Eintracht Frankfurt kwenye Dimba la Wirsol Rhein-Neckar.

Eintracht Frankfurt wapo vizuri sana kwa msimu huu wakiwa wanapewa nafasi kubwa ya kuwa kati ya zile timu nne za juu kutokana na kiwango ambacho wamekuwa wakikionyesha kwenye michezo yao.

K w a s a s a wapo katika nafasi ya saba w a k i w a wamekusanya pointi 18 kibindoni, wamekuwa wakipambana sana na wameshashinda michezo mitano, wametoka sare mitatu na kupoteza mitatu lakini wanaaminika kuwa wanaweza kutikisa kwenye mechi hii. Kabla ya mechi hizo, Ijumaa kutakuwa na kipute cha juu sana wakati wabishi Stuttgart watakapovaana na wanaume wa shoka Borussia Dortmund kwenye Uwanja wa MercedesBenz-Arena.

Dortmund wakishinda moja kwa moja watasogea hadi nafasi ya pili kwenye ligi hiyo na kusubiri matokeo ya wikiendi kuona kama watashushwa tena na Leipzing ambao watakuwa wakitakiwa kushinda dhidi ya Bayern Leverkusen ambao nao wamekuwa bora sana msimu huu.

Dortmund watakuwa wanamtegemea staa wao PierreEmerick Aubameyang ambaye hadi sasa anashika nafasi ya pili kwenye chati ya ufungaji akiwa amefunga mabao 10, moja nyuma ya Robert Lewandowski mwenye mabao 11.

No comments:

Powered by Blogger.