Trending News>>

MICHEZO:Romario adai yeye alikuwa bora zaidi ya Maradona na Messi ila NEYMAR ni zaidi kwasasa.

ROMARIO ADAI YEYE ALIKUWA BORA ZAIDI YA MARADONA NA MESSI, ILA NEYMAR KWA SASA NI ZAIDI…

Mjadala wa mchezaji bora wa Dunia umeamka upya baada ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona. 
 Romario kuibua mapya baada ya mechi ya el clasico kumalizika kwa Barca kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Real Madrid. 
Lakini mjadala huu ulizua utata baada ya jina la Cristiano Ronaldo kutojumuishwa katika mjadala huo. Romario aliwataja wachezaji wawili toka Argentina ambao wote wamecheza klabu ya Barca. romario aliwataja Diego Maradona na Lionel Messi. 
Romario alisema “Messi hajabeba World Cup na itamlazimu kufanya hivyo ili awe bora. Kwa hio ni wazi kuwa Armando Maradona ni bora zaidi ya Messi”. Romario aliiambia FOX Sports ya nchini Brasil. 
Akaenda mbali zaidi kwa kusema Kuwa pindi yeye alipokuwa uwanjani alikuwa ni bora ya wawili hao Kwa namna yoyote ile uwanjani, na hilo nalisema nikiwa na uhakika wa asilimia 100 pasipo na hofu yoyote ile. 
Lakini pia Romario aliusifu pia uwezo wa Messi baada ya ushindi muhimu walioupata mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu, huku Messi akiliweka jina lake kwenye anga la juu na hata kuweza kuchaguliwa tena kuwa mwanasoka bora ajae wa Dunia. 
Romario alimalizia kwa kuamsha utata baada ya kusema “hii leo ukiangalia kwa jinsi anavyocheza akiwa na klabu na hata timu ya taifa, nampa heshima ya mwanasoka bora wa Dunia  Neymar”. 
Alimaliza Romario.

No comments:

Powered by Blogger.