VITA YA NBA NI OKTOBA 17, NI CURRY VS LEBRON
Lebron James
Mashabiki wanawasubiri mastaa kama Lebron James na Steven Curry kama watapata nafasi ya kuendelea kuonyesha umwamba wao msimu huu. Hata hivyo, maombi ya timu nyingi ya kuwa na mapumziko kipindi cha Sikukuu ya Krismasi yaani Desemba 25 na 26, yametupwa na sasa siku hiyo kutakuwa na mechi tano ambapo tatu zitaonyeshwa Live na mbili zitarekodiwa.
Mchezo ukiendelea.
Sherehe hizo zitaanza tarehe hiyo kwa mabingwa watetezi Golden State Warriors kutambulisha kombe lao walilotwaa msimu uliopita kwa mashabiki wao na baadaye watakawaribisha Houston Rockets ambao watakuwa na staa wao mpya Chris Paul, ambaye atacheza mchezo wake wa kwanza na timu hiyo. Paul anapewa nafasi kubwa ya kufanya maajabu kwenye msimu huu kwa kuwa ni kati ya wachezaji bora zaidi kwenye kipindi cha NBA
kilichopita.
Pia staa Gordon Hayward, anatarajiwa kuitumikia timu yake Boston Celtics kwenye mchezo wake wa kwanza wakati itakapovaana na mastaa waliofika fainali msimu uliopita, Cleveland Cavaliers. ESPN msimu huu watakuwa wakionyesha michuano ya NBA, kwa mara yao ya 16 wakitajwa kama televisheni ambayo imekuwa ikionyesha mchezo huu kwa mafanikio makubwa zaidi na sehemu kubwa ya dunia.
Wengine ukiachana ESPN na Kwese ambao watakuwa wakionyesha michuano hiyo kwa upande wa Afrika, TNT nao ni kampuni ambayo inapewa nafasi kubwa ya kuwika ikiwa inatajwa kuwa itaonyesha mchezo wa kwanza wa NBA kati ya Oklahoma City Thunder ambayo itakuwa na staa wake Paul George ambao watawakaribisha New York Knicks, lakini pia wataonyesha mchezo kati ya LA Clippers watakaovaana na Los Angeles Lakers kwenye mchezo wao wa pili. NBA, wametangaza kutakuwa na michezo mitano siku ya tarehe 25 Desemba, ikiwa ni mwaka wa kumi mfululizo, lakini kwa mara ya kwanza ABC watakuwa wakionyesha michezo mitatu Live.
No comments:
Post a Comment