Trending News>>

Real Madrid waichapa tena Barcelona na kubeba kombe

Mabao 3 ya mwisho ambayo Marco Asensio amewafungia Madrid ameyafunga katika michezo ya fainali, na jana dakika ya 4 tu aliendeleza rekodi hiyo baada ya kuwafunga Barcelona.
Asensio alifunga bao hilo kwa shuti kali nje ya box dakika ya 4 kabla ya Karim Benzema dakika ya 39 kuipatia Real Madrid bao la pili na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko huku ubao wa matokeo ukiwa mbili kwa Madrid na Barca sifuri.
Kipindi cha pili hakukuwa na mabadiliko ya matokeo kwani mabao hayo mawili yalidumu hadi mwisho wa mechi, mchezo huo uliopigwa Santiago Bermabeu ulikuwa wa pili kwani wa kwanza ulishapigwa katika uwanja wa Nou Camp wakati Real Madrid wakishinda 3 kwa 1.
Katika mchezo huo mshambulia anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu Cristiano Ronaldo alionekana jukwani akiwa na mpenzi wake Georgina, Ronaldo amefungungiwa katika michezo mitano baada ya kumuonesha muamuzi vitendo visivyo vya kiungwana.
Kipigo cha Barca kimemfanya kocha Ernesto Velvarde kuwa kochwa wa pili baada ya Luis Aragones 1987 kupokea vipigo viwili mfululizo katika mechi za ufunguzi wa ligi huku bao la Benzema likimfanya kuwa mchezaji wa 8 katika orodha ya wafungaji Madrid mda wote akiwa na mabao 181.

No comments:

Powered by Blogger.