Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’
HIT MAKER wa ngoma inayobamba kwa sasa Acheze, Emmanuel Elibariki
‘Nay Wa Mitego’, amesema aliumizwa sana na maneno ya rapa mwenziye, Roma
Mkatoliki, aliyeongea maneno ya kumkashifu mara baada ya kuibuka baada
ya kutekwa kwake, miezi michache iliyopita.
NAY WA MITEGO AFUNGUKA…
“Roma anatakiwa ajue kwamba mimi ni mmoja kati ya
wasanii
ambao walishinda kutwa nzima kwenye studio yake ya Tongwe Records na
kituo cha polisi, toka siku aliyotekwa hadi siku aliyopatikana, lengo
likiwa ni kutaka kujua tunasaidiana vipi ili aweze kupatikana.
Roma Mkatoliki.
“Akitaka kuthibitisha hilo amuulize mkewe, lakini nikashangaa baada
ya kupatikana eti akanikashifu, kila nikikumbuka inaniumiza, sema mimi
ni mwanaume siweki vitu
rohoni, na pia nimeipenda sana ngoma yake ya Zimbabwe, Roma ni rapa mkali, sina kipingamizi juu ya hilo,” amesema Nay Wa Mitego.
No comments:
Post a Comment