Hamadi All ‘Madee’
BAADA ya kumwagiwa mkwara mzito, Rais wa Manzese
ambaye pia ni mkali katika Muziki wa Bongo Fleva, Hamadi All ‘Madee’
amefungukia ishu ya kuchambwa na msanii wa filamu Bongo, Jacqueline
Wolper kuwa alikuwa sahihi kumchamba kwa kuwa alitumia picha ya katuni
inayofanania na yeye bila kumuomba.
Madee afungukia kuchambwa
Akizungumza na Showbiz, Madee alisema, wakati wa kutengeneza video
yake mpya ya Sikila aliyomshirikisha staa kutoka Nigeria, Tekno yenye
muonekano wa kikatuni, mchoraji alipendekeza kutumia msichana mweupe na
mwenye sifa tofautitofauti hivyo wazo likamjia la kumtumia Wolper.
“Nilikosea kumtumia Wolper kwa sababu kwanza sikumuomba.
Wolper.
Wolper ni mshkaji nitawasiliana naye
ili tuweze kulimaliza,” alisema Madee. Juzikati kupitia ukurasa wake wa
Instagram, Wolper alimchamba Madee kwa kumtumia muonekano wa kikatuni
katika wimbo wake.
MADEE afungukia kuchambwa na Wolper
Reviewed by
Unknown
on
August 18, 2017
Rating:
5
No comments:
Post a Comment