Mwanafunzi ahukumiwa miaka 20 jela kwa kukutwa na picha za ngono.
Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma
mjini Tabora, Marick Mbega amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20
jela baada ya kutiwa hatiani kudhalilisha wanafunzi wa Shule ya Msingi
Isike.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, Emanuel Ngigwana baada ya
kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka wakiwamo
wanafunzi wiwili waliodhalilishwa.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Wakili wa
Serikali, Upendo Malulu alidai mahakama Marick alitenda makosa hayo
AprilI 4, mwaka huu kinyume na kifungu namba 138 A cha kanuni za adhabu
sura ya 16 ya 2002.
Wakili huyo aliendelea kusema mahakamani hapo
kwamba mtuhumiwa huyo aliwaonyesha wanafunzi wa shule hiyo picha za
kongo kwa kutumia simu yake ya mkononi jambo ambalo alijua ni kinyume na
sheria pamoja na maadili ya kitanzania.
Mtuhumiwa huyo inaelezwa kuwa hakuishia
katika kuwaonyesha wanafunzi hao picha hizo bali aliwashawishi wanafunzi
hao wamshike sehemu za siri huku na yeye akiendelea kuwachezea.
Ndani ya simu ya mkononi ya Mbega, Wakili
Malulu aliiambia mahakama kuwa walikuta picha 197 za ngono na video 40
za wanyama, watoto na watu wazima baada ya kuifanyia upekuzi.
Hakimu alisema kitendo alichokifanya Mbega
kinachukuliwa kama udhalilishaji kwa sababu watoto hawana maamuzi hivyo
hawawezi kuchukuliwa kama walikubali kutazama picha hizo pamoja na
kuchezewa sehemu zao za siri. Watoto wanatakiwa kukukuwa salama
kamaadili, kiakili hivyo kuwaonyesha picha za ngono na kuwachezea sehemu
za siri ni kuwadhalilisha.
Upande wa mashtaka uliiomba mahakama itoe
adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye
tabia za kudhalilisha watoto katika jamii.
chanzo: swahili times.
No comments:
Post a Comment