BILIONEA NEYMAR AWEKA REKODI YA DUNIA
Habari ni kuwa mshahara wake unatajwa utakuwa ni pauni 596,000 (Sh bilioni 1.7) kwa wiki huku yeye mwenyewe akikabidhiwa pauni 45m (Sh bilioni 131) kama ya uhamisho wake, ukijumlisha na mengine mengi inaelezwa gharama nzima ya kumsajili ni pauni 398m (Sh trilioni 1).
Dili hilo limefi kia hapo ambapo awali kabisa baba Neymar ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mwanaye alipokutana na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ambaye ni bilionea, hapo ndipo kila kitu kilipomalizika. Wakala Wagner Ribeiro ambaye anafanya kazi na Neymar alinukuliwa akisema jana jioni kuwa ada hiyo italipwa ndani ya saa 48 na kisha leo Ijumaa Neymar atatua Paris kukamilisha dili.
Ikiwa dili la Neymar litakamilika kwa ada hiyo, atakuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa mara mbili ya lile linaloshikilia rekodi kwa sasa. Mbali na usajili huo inaelezwa kuna mchakato unafanyika kumpa Neymar mkataba wa pauni 269m (Sh bilioni 788) kwa miaka mitano ili kupromoti michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Qatar mwaka 2022.
Uhamisho huo unaonekana kuwa unaweza kuwa mbaya kibiashara kwa Barcelona na Hispania kwa jumla. Muda mfupi baada ya kujulikana anaondoka, mabango yenye taswira ya Neymar akiwa na jezi ya Barcelona yaliondolewa sehemu mbalimbali. Aidha, taarifa zingine zilieleza kuwa uongozi wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, jana mchana ulipinga kupitisha kiasi hicho cha fedha za usajili kwa kudai ni kikubwa na kikakiuka misingi ya matumizi ya fedha za soka.
No comments:
Post a Comment