Waziri Mkuu Azisifu Taasisi za Agha Khan......Asisitiza Tanzania ni Salama Kwa Uwekezaji
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji
watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani,utulivu wa
kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.
Ameyasema
hayo jana Julai 09,2017 alipomuwakilisha Rais Dkt.John Magufuli katika
maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu
Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.
Waziri
Mkuu alisema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini,
hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.
Aliupongeza
mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt.Magufuli
katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini
kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
"Nawahakikishia
kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa
sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba
muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia
popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo", Majaliwa.
Kwa
upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw.
Amin Lakhani aliishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba
ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali
nchini.
Alisema
mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za
afya,elimu,kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia
kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji
ili kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment