WABUNGE 6 WA CHADEMA WAHOJIWA KWA KUMSHAMBULIA MBUNGE WA CCM
Wabunge
sita wa Chadema usiku wa kumkia leo wamehojiwa na polisi kwa tuhuma za
kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza.
Mwenyekiti
mwenza wa wabunge wanaounda umoja wa katiba (Ukawa) James Mbatia
amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga, Saed
Kubenea(Ubungo), Pauline Gekul (Babati Mjini), Frank Mwakajoka
(Tunduma), Joseph Selasini (Rombo) na Cecilia Pareso (Viti Maalum).
Hadi
saa 5.00 usiku wabunge hao bado walikuwa wakiandika maelezo katika
kituo cha polisi. Wabunge hao ni kati ya wabunge wanane waliotajwa na
Spika wa Bunge Job Ndugai alipokuwa akiahirisha kikao cha bunge jioni
kuwa wanatuhumiwa kumshambulia Shonza.
Wabunge
wengine waliotajwa katika sakata hilo lililotokea Jumatatu mchana
mchana katika lango la kuingilia jengo la utawala ni Devotha Minja (Viti
Maalum) na Cecil Mwambe (Ndanda).
Hata
hivyo James Mbatia alipohojiwa Saa 5.45usiku alisema kuwa wabunge hao
waliachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano na kutakiwa kurud polisi
Jumanne Saa 3 asubuhi.
Hata hivyo Mbatia ameshangazwa na kitendo cha kutajwa kwa Mwambe ambaye amesema hii ni wiki ya pili hayupo mjini Dodoma.
“Mimi
nilikuwa msimamizi wa kambi yetu, Mwambe aliniaga tangu wiki mbili
zilizopita anaenda jimboni na hajarudi sasa tunashangaa kutajwa
alikuwepo wakati wa tukio,” amesema.
Wabunge hao walidakwa mmoja mmoja na askari waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia (askari kanzu) wanaolinda bunge.
Kukamatwa kwa wabunge hao kulifuatia Shonza kwenda kushtaki kwa Ndugai naye kutoa kibali cha kukamatwa kwa wabunge hao.
No comments:
Post a Comment