TUNDU LISSU AACHIWA KWA DHAMANA
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini, Tundu Lissu
mapema leo asubuhi.
Lissu
ametakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja ataweka
bondi ya dhamana ya shilingi milioni 10 huku akiwekewa zuio la kutoka
nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali maalum cha mahakama.
Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini.
Tundu
Lissu ambaye alikamatwa Alhamisi, Julai 20 mwaka huu, katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akijiandaa kuelekea
Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Chama cha Wanasheria cha Afrika
Mashariki (EALS), alifikishwa Mahakamani hapo Jumatatu Julai 24 na
kusomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, kosa
ambalo anadaiwa kulitenda Julai 17.
Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alipotakiwa
kukubali ama kukataa makosa hayo na Hakimu Mashauri, Lissu alisema
kusema kweli haijawahi kuwa kosa la jinai. Mahakama ya Kisutu ilimnyima
dhamana Tundu Lissu, kesi iliahirishwa hadi leo Julai 27, 2017 ambapo
amepewa dhamana.
No comments:
Post a Comment