Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos atangazwa tajiri namba 1 duniani baada ya kumpita Bill Gates leo
Mwanzilishi
wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos amempita Bill Gates na kuwa tajiri
namba moja duniani akimiliki utaji wa dola za kimarekani 90.6 bilioni
(Tsh 203 trilioni).
Kupanda
wa hisa za Amazon kwa asilimia 1.5 leo Alhamisi Julai 27 kulimaanisha
kuwa tajiri huyo amempita mwanzilishi mwenza wa Microsoft, kwa mujibu wa
taarifa za jarida la Forbes la nchini Marekani.
Forbes
wameeleza kuwa Bezos ana utajiri wa $90.6 bilioni akimzidi Bill Gates
aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa na utajiri wa $90 billioni sawa
na Tsh 201.5 trilioni.
Bezos ananakadiriwa kumilikia hisa milioni 80 za Amazon akiwa ni mwenye hisa nyingi zaidi ya mwingine yeyote.
Kwa
miaka ya hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika mradi wake wa
Blue Origin unaohusika na urushaji wa rocket kwenda angani pamoja na
Washington Post ambazo zote anazimiliki.
Bezos
ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (CEO) wa Amazon
alizaliwa mwaka 1964 Albuquerque Jimbo laNew Mexico na alisoma Sayansi
ya Kompyuta na Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Princeton.
Alipohitimu
alikwenda kufanya kazi na Wall Street lakini mwaka 1994 aliacha kazi na
kwenda kuanzisha Amazon ambapo kwa mara ya kwanza Amazon ilianzishiwa
katika karakana ya kutengenezea magari. Baada ya kampuni hiyo kuanza
kufanikiwa na kujipanua katika nchi mbalimbali, mwaka 2000 alianzisha
kampuni ya Blue Origin inayojishughulisha na masuala ya anga.
Mwaka
2013 akiendelea kujipanua, aliinunua Kampuni ya Washington Post kwa
$250 milioni na ilipofika Mei 2017 alitajwa kuwa na utajiri wa $ 84.8
bilioni, lakini leo Julai 27, 2017 amefikisha utajiri wa $90.6 bilioni
na kushikilia usukani wa mtu tajiri zaidi duniani.
Kwa mujibu wa Forbes, hawa ndio matajiri 10 wanaoongoza duniani;
- Jeff Bezos (53)- Amazon.com
- Bill Gates (61)- Microsoft
- Amancio Ortega (81)- Zara
- Warren Buffett (86)- Berkshire Hathaway
- Mack Zuckerberg (33)- Facebook
- Carlos Helu (77)- telecom
- Larry Ellison (72)- software
- Michael Bloomberg (75)- Bloomberg LP
- Bernard Arnault (68)- LVMH
- Charles Koch (81)- diversified
No comments:
Post a Comment