Tanzania ni salama kwa Uwekezaji- Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa
kuwa Tanzania ni nchi yenye amani,utulivu wa kisiasa na uchumi wenye
kukua kwa kasi.
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.
Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt.Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
"Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo", Majaliwa.
Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.
Amesema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya,elimu,kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment