Trending News>>

Sihitaji 'Coming Soon' - Barnaba


Mwalimu na mwanamuziki wa Bongo  Fleva, Barnaba Classic amesema kilichomfanya asitangaze ujio wa wimbo wak mpya 'Tunafanana' ni baada ya kugundua  watanzania wamechoka kusubirishwa kwa kazi zisizo na ubora.
Akizungumza kwenye FNL ya EATV Barnaba amedai kuwa baada ya kuangalia nyimbo nyingi zilizotoka hivi karibuni kwa kupigiwa matangazo nyingi zilikua mbovu kitu ambacho mashabiki wengi kimekuwa kikiwachosha.
"Wasanii wamekuwa na coming soon nyingi sana, alafu nyimbo zao zinakuwa mbovu. Hii inaharibu mind set za mashabiki, na sas a hivi ukipiga kelele kwamba wimbo mpya coming soon mashabiki wanaona ni yale yale ndiyo maana mimi nikaamua tuu kuachia kazi  bila kelele na inafanya vizuri imepokelewa vizuri sana kuliko zinazosumbua kupigiwa kelele", Barnaba
Aidha Barnaba ameongeza kwamba "Acha kazi zangu zipige kelele zenyewe. Mimi watu watanijua kupitia kazi na siyo kelele.  Unajua kuna kitu kinatwa 'Superstar' alafu kuna Maarufu. Superstar ni pale watu wanapokujua kupitia kile ambacho unakifanya na watu wakakujua kupitia hicho kitu lakini Umaarufu ni pale ambapo unajulikana kuliko kazi yani kelele tupu, hivyo mimi na kaa kundi la kujulikana kupitia kazi yangu ya muziki na siyo kelele ",  Barnaba aliongeza

No comments:

Powered by Blogger.