Taarifa ya Watumishi vyeti feki kurudi kazini
Wafanyakazi zaidi ya 450 ambao walisimamishwa kazi na kusitishiwa
mishahara yao kwa tuhuma za kuwa na vyeti feki wamerudishwa makazini
baada ya kushinda rufaa zao.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa watumishi hao 450 ni kati ya
watumishi 1500 ambao walikata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya serikali ya
kutaka watumishi wenye vyeti feki kuacha kazi na kusitishiwa mishahara
yao.
"Kati ya hao wengine walikuwa ni wale ambao wameolewa na kupata majina
ya waume zao kwa hiyo baada ya kuolewa majina ya wanaume zao yakawa
yanatofautiana na majina yao yaliyopo kwenye vyeti, kwa hiyo wakati ule
vilikuwa vinaonekana vile vyeti kama si vyao na kwa bahati mbaya
Watanzania wanapoolewa wanachukua majina mawili ya wanaume zao badala ya
kuchukua jina moja. Lakini pia kulikuwa na wengine majina yao ya kidato
cha nne na kidato cha sita yalikuwa tofauti" alisema Ndumbaro
Mwanzoni wa mwezi wa tano mwaka huu serikali ya Tanzania ilitangaza
kuwafuta kazi zaidi ya watumishi 9,932 ambao walibainika kuwa na vyeti
feki na baadaye zaidi ya watumishi 1500 walikata rufaa kupinga maamuzi
hayo ya serikali kwa kusema hawana vyeti feki, hivyo zaidi ya watumishi
400 wamethibitika kweli kutokuwa na vyeti feki na sasa watarudi makazini
na kuendelea na majukumu yao...
No comments:
Post a Comment