Taarifa ya serikali kuhusu watumishi waliokata rufaa ya vyeti feki
WATUMISHI WA UMMA WALIOKATA RUFAA KUHUSU UHALALI WA VYETI
Watumishi
wa umma waliowasilisha vyeti vyao vya kuhitimu kidato cha nne, cha sita
na ualimu kwa ajili ya rufaa katika Baraza la Mitihani la Taifa (NETA)
kuhusu zoezi la uhakiki, wanatakiwa kuwasiliana na waajiri wao ili
kupewa matokeo ya hatma ya rufaa kuhusu uhalali wa vyeti vyao.
Ipo
taarifa inayosambaa katika mitandao mbalimbali ikiwa ni majina ya
wanaodaiwa kuwa watumishi wa umma na maeneo yao ya kazi ikiwa na
kinachodaiwa matokeo ya rufaa zilizokatwa kuhusu uhalali wa vyeti vya
elimu kwa wahusika. Wananchi na watumishi wote wanaelezwa kuwa, serikali
inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa na mawasiliano.
Taarifa inayosambazwa haijatolewa na serikali na ipuuzwe.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali,
Ofisi ya Rais-Utumishi,
08.07.2017
No comments:
Post a Comment