TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA
- DEREVA NA KONDAKTA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI WILAYANI MISUNGWI.
KWAMBA TAREHE 06.07.2017 MAJIRA YA SAA
12:30HRS KATIKA BARABARA YA MWANZA KWENDA SHINYANGA KIJIJI CHA MISUNGWI
KATA NA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI AMBAO NI DEREVA
NA KONDAKTA WA GARI LENYE NAMBA T.574 AZU AINA YA SCANIA BUS MALI YA
KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS , WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.SUDI YUSUPH
MIAKA 35, DEREVA WA BUS LA KAMPUNI YA BUNDA EXPRESS, MKAZI WA BUZURUGA
–MWANZA NA 2.BONIPHACE MASHAURI, MIAKA 52, KONDAKTA WA BUS LA KAMPUNI YA
BUNDA EXPRESS, MKAZI WA MUSOMA – MARA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
KWA KOSA LA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA “MIRUNGI” KIASI CHA
MABUNDA 112, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI POLISI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA
RAIA WEMA KWAMBA BUS TAJWA HAPO JUU LINALOFANYA SHUGHULI YA KUSAFIRISHA
ABIRIA KUTOKA MUSOMA KWENDA DODOMA LINAJIHUSISHA PIA NA KUSAFIRISHA
MADAWA YA KULEVYA (“MIRUNGI”). AIDHA BAADA YA ASKARI KUPATA TAARIFA
HIZO WALIWEKA MTEGO, NDIPO JANA TAREHE TAJWA HAPO JUU BUS HILO LIKIWA
LINATOKEA MUSOMA KWENDA DODOMA LILIPOFIKA KIJIJI CHA MISUNGWI ASKARI
WALILISIMAMISHA KISHA LIKAFANYIWA UPEKUZI NA KUKUTWA LIKIWA LIMEBEBA
MIRUNGI AMBAYO NI KUNDI LA MADAWA YA KULEVYA KIASI CHA BUNDA 112,
YALIYOKUWA YAMEHIFADHIWA NDANI YA MABEGI KISHA KUWEKWA NDANI YA BUTI YA
GARI.
MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE NI UTINGO WA GARI
HILO AMETOROKA, JUHUDI ZA KUMTAFUTA BADO ZINAENDELEA. POLISI WAPO KATIKA
UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
WATUHUMIWA WOTE WAWILI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA UCHUNGUZI NA MSAKO
WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE
KATIKA UTUMIAJI, UUZAJI NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KATIKA MKOA
WA MWANZA BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU
KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA
MOTO HUSUSANI WAMILIKI WA MABASI KUACHA KABISA TABIA YA KUJIHUSISHA NA
USARISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA KWANI NI KOSA LA JINAI NA ENDAPO GARI
LITAKAMATWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHULIWA DHIDI YA MWENYE MALI.
AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WAHALIFU
NA UHALIFU MAPEMA ILI WATUHUMIWA WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE
VYOMBO VYA SHERIA.
No comments:
Post a Comment