MREMBO SANCHI MAHARI YA MILIONI 10
JANE
Rimoy, ni jina la msanii ambaye amejizolea umaarufu mkubwa katika
viunga vya burudani Bongo baada ya kuonekana kufanya vizuri katika
kupamba video vya wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, au kama wenyewe
tunavyosema, Bongo Fleva. Hata hivyo, mashabiki hao wanamfahamu zaidi
kwa jina lake la Sanchoka au Sanchi!
Umbo
lake kubwa limemfanya kuwa kivutio, ingawa mara kadhaa wadau wamekuwa
wakihoji uhalali wa mwili wake, wakihofu kuwa huenda anatumia madawa ya
kuongeza ukubwa, ambapo hapa kwetu zinafahamika zaidi kama Mchina.
Kabla
ya kukutana naye ana kwa ana, hata mimi nilikuwa na hisia hizo, lakini
nilipomtia machoni na kufanya naye mazungumzo kuhusu mwili wake, niliona
kuwa ni mwili wake kweli. Binti amekaa vizuri.
Kwa wanaume wadhaifu wa miili mikubwa ya akina mama hasa makalio, hapa wanapata presha.
Kuna
wakati mmoja, picha zake zilitembea katika mitandao mingi ikimuonyesha
akichezesha makalio yake kwa namna ambayo haikuwa nzuri.
Hiyo tisa, lakini hivi majuzi Sanchoka ametoa kauli ambayo imetembea
sana huko mitandaoni na kwa vile hakujitokeza kukanusha, ni wazi ilikuwa
ni yake na alidhamiria kupeleka ujumbe kwa mashabiki wake.
Kuna
kauli alisema mwanaume anayetaka kumuoa, basi ni lazima ajipinde na
kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi taslimu kama mahari yake! Ndiyo,
shilingi milioni kumi kama mahari! Lakini hakuacha kufafanua, alisema
anaona kiasi hicho anastahili ili kumfanya mwanaume atakayemuoa na
kummiliki, atambue thamani yake, kwani wanawake wengi wamekuwa
wakinyanyasika baada ya kuolewa kwa vile huolewa kwa mahari ndogo ambayo
haifanani na wao.
Ni
kweli kwamba mwanamke anapaswa kujitambua thamani yake na hata
kumweleza kwa maneno au hata kwa vitendo mwenza wake, lakini staili hii
ya Sanchoka, kutaja kiwango cha fedha siyo sawa. Mahari ya milioni 10
kwani umekuwa ng’ombe? Kwanza nimwambie kuwa, utu hata siku moja
haujawahi kuwa na kiwango cha fedha, yaani hakuna mkwanja wowote ambao
unaweza kuthaminishwa na mtu! Watu wengi wanataja viwango vya fedha kama
thamani zao kutegemea na nini wanafanya.
Kwa
mfano, kama Sanchoka atataka kupewa kiasi cha shilingi milioni tatu kwa
mfano, ili atokee kwenye video ya msanii f’lani, ni sawa, kama ambavyo
mwanasoka anavyotaka fedha za usajili kulingana na kiwango chake cha
uchezaji uwanjani.
Lakini
mtoto wa kike unapotaja kiasi cha fedha ambacho mtu anayetaka kuwa
mumeo inabidi atoe, inaleta ujumbe mwingine tofauti kabisa. Kwa namna
ambavyo Sanchi amejitengeneza machoni mwa mashabiki, maneno
aliyoyaandika yana tafsiri nyingi, lakini kwa namna alivyotaka watu
waelewe, inaleta shida kidogo.
Kama
ni thamani ya utu wa mwanamke, haupatikani kwa kiwango cha fedha, kwa
sababu kuna watu wana fedha, wanaweza kutoa na kumpatia, lakini kamwe
asipate heshima ambayo yeye anadhani anayo. Na mwanaume hata siku moja
hapati thamani ya mwanamke kwenye fedha, kwa sababu kama ni mtu
anayependa fedha humtumia kama chombo cha starehe tu.
Mwanaume
anayehitaji mwanamke wa kumweka ndani, huogopa sana kuchukua wanawake
dizaini ya Sanchoka, kwa sababu wanaamini katika fedha.
Maana,
hata kama akipatikana bwana mwema anayeweza kuwa na msaada mkubwa
kimaadili, hana nafasi kwa Sanchi kwa sababu tu hana kitu? Anaweza
kupata wanaume wengi wenye kiasi hicho cha fedha, lakini kitu ambacho
ninaweza kumhakikishia ni kuwa itamchukua miaka mingi sana kumpata mume
bora wa ndoa. Watu watatoa pesa, ili wapate wanachovutiwa kutoka kwake
halafu wataendelea na maisha mengine, siku atakayokuja kushtuka, umri
ushamtupa mikono na hakuna tena mtu wa kumtamani kama mke.
No comments:
Post a Comment