Ronaldo akimbia waandishi mahakamani
Nyota wa
timu ya taifa ya Ureno na Real Madrid ya nchini Hispania, Cristiano
Ronaldo amevikwepa vyombo vya habari baada ya kuwasili mahakamani kwa
mara ya kwanza hii leo.
Ronaldo
anayekabiliwa na tuhuma za kukwepa kulipa mamilioni ya fedha kwaajili ya
kodi amefika mahakamani hapo huku akikataa kuzungumza na vyombo vya
habari.
Cristiano
Ronaldo, ambaye anakanusha kutennda kosa lolote alitarajiwa kutoa
taarifa baada ya kuhudhuria kesi katika mahakama huko Pozuelo de Alarcon
mahala ambapo ndipo anapoishi.
Lakini
mara baada ya kuwepo mahakamani hapo aliamua kutozungumza chochote na
waandishi baada ya kikao chao kilichodumu kwa takribani dakika 90 na
wakili wa kampuni yake, Inaki Torres akizungumza kwa niaba yake
amesistiza kuwa “ Kila kitu kipo chini ya uangalizi”.
Waendesha
mashitaka wanasema Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, anashutumiwa
kukwepa kodi yenye thamani ya Euro milioni 14.7 ikitokana na haki ya
matangazo kunako mwaka 2011 na 2014.
Endapo
mshindi huyo mara nne wa Ballon d’Or atakutwa na hatia katika kesi hiyo
inayo mkabili atalazimika kulipa faini ya Euro milioni 28 na kifungo cha
miaka mitatu na nusu jela.
No comments:
Post a Comment