MSICHANA KUFUNGWA JELA MIAKA 10 KWA KUDANGANYA KUWA AMEBAKWA
Msichana mkazi wa Texas, Marekani ambaye alikimbilia Kanisani na kudai
kuwa amebakwa na kundi la Wanaume watatu wenye asili ya Afrika, huenda
akahukumiwa kifungo jela baada ya kukiri kwamba alidanganya.
Breana Harmon, mwenye umri wa miaka 19, mapema mwezi March alikimbilia
Kanisani mjini Denison, Texas, akiwa na nusu uchi na mwili wake ukiwa
damu na kudai kubakwa na wanaume wawili wakati mwingine akimshikilia
chini, unaripoti mtandao wa KXII.
Hata hivyo, vipimo vya Hospitali havikuonesha ushahidi wowote kuwa
msichana huyo alidhalilishwa na wanaume hao wenye asili ya Afrika ambapo
wiki mbili baada ya tukio hilo alikiri kwa Polisi kuwa alidanganya juu
ya tukio hilo na kuumia kwake kulitokana na yeye mwenyewe.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Joe Brown, msichana huyo alifunguliwa kesi ya
jinai mapema wiki hii kutokana na kudanganya ambapo thamani ya kosa ni
kifungo cha hadi miaka 10 jela na faini ya Dollar 10,000.
“Tulivyoangalia katika kilichotokea kwenye kesi hii, na kuzingatia
madhara iliyosababisha, na pengine itakayosababisha, tunaamini
alichokifanya kinastahili adhabu zaidi. Alichokifanya ni kikubwa, na
tunaamini ilikuwa ni kosa la jinai.” – Joe Brown.
No comments:
Post a Comment