Trending News>>

Mwalimu amtwanga Manny Pacquiao



Manny Pacquiao anaonekana kuendelea kupokea vichapo, na sasa amepokea kipigo kutoka kwa Jeff Horn ambaye kabla ya kuwa bondia alikuwa ni mwalimu katika pambano la raundi 12 lililopigwa nchini Australia.

Jeff Horn alionekana kumshambulia Manny Pacquiao kuanzia raundi ya kwanza ya mpambano huo, japokuwa mwanzo Pacquao alionekana kujaribu kujitetea.

Pacquiao alionekana kuzidiwa zaidi kadri pambano lilivyokuwa likiendelea kwani ngumi alizokuwa akipigwa na Horn zilionekana kumchana pembeni ya jicho.

Pamoja na kushambuliwa sana lakini ilipofika raundi ya 9 Horn alionekana kuanza kupata tabu kutokana na ngumi za kushtukiza na za haraka zilizokuwa zikirushwa na Pacquiao.

Baada ya mpambano huo kura za majaji watatu zilimpa ushindi Horn kwa alama 117-111, 115-113 na 115-113 na kumfanya Horn kuwa bingwa wa WBO WORLD WELTERWEIGHT.

Pacquiao 38 ambaye ni raia wa nchini Ufilipino kwa sasa anakuwa amepoteza mapambank manne kati ya tisa aliyocheza mara ya mwisho hii ikiwa ni rekodi mbaya sana kwake.

No comments:

Powered by Blogger.