Trending News>>

Mume Wangu Anaota Na Kutaja Jina La Dada Wa Kazi

Mume wangu ana tabia ya kuongea usingizini na mara nyingi huwa simsikilizi, lakini kwa muda wa kama siku tatu hivi akilala amekuwa akitaja jina la dada wa kazi hapa nyumbani.

Sijawahi kuwahisi chochote sababu mara nyingi dada anakuwa chumbani kwake mume wangu akiwepo nyumbani. Hawana mazoea ya kuwa sehemu moja pamoja. Nimekua na dada huyu wa kazi kwa muda wa mwaka mmoja. Sio binti mdogo ni mdada tu wa kawaida.

Nimeshindwa kumuuliza mume wangu kwa sababu sijui kama kuna kitu kinaendelea kweli au hakuna kinachoendelea. Sijui cha kufanya. Tumekua kwenye ndoa kwa muda wa miaka 3 na mume wangu hajawahi kunisaliti hata mara moja, sijawahi kumfumania au kuona au hata kusikia chochote.

Naomba ushauri jamani

No comments:

Powered by Blogger.