Trending News>>

MSANII JUSTIN BIEBER AANDAMWA NA MIKOSI


Msanii wa muziki Justin Bieber amekuwa akiandamwa na mikosi baada ya kukatazwa kufanya tamasha lake nchi China.
Siku ya jana msanii huyo alijikuta akimgonga na gari mpiga picha mwenye miaka 57 baada ya kutoka kanisani. Tukio hilo limetokea maeneo ya Beverly Hills nchini Marekani.

Msanii huyo alijikuta akipatwa na hofu baada ya kumgonga kwa bahati mbaya mtu huyo hali iliyopelekea kutoka katika gari na kumuhoji aliyemgonga anataka nini ili aondoke eneo la tukio.
Hata hivyo dakika chache Polisi wa Sgt. Matthew Stout waliwasili eneo la tukio na kumsaidia msanii huyo kutoa msaada kwa majeruhi ambaye alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu baada ya kupata majeraha.

No comments:

Powered by Blogger.