Mahakama ya ICC Yaituhumu Afrika kusini
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeamua kuwa Afrika
Kusini, ilifanya makosa kwa kutomkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir
wakati alifanya ziara nchini humo mwaka 2015
Ilisema kuwa Bashir hakuwa na kinga ya kidiplomasia na hivyo angekamywa
na kukabidhiwa kwa mkuu wa mashtaka kwa wa ICC kufuatia madai ya
kuhusika kwenye mzozo wa jimbo la Darfur.
Serikali ya Rais Jacob Zuma, imesema kuwa masharti ya ICC yanaenda
kinyume na sheria za nchi na kuwa imeanzisha mchakato wa kuondoka kutoka
uanachama wa ICC, hatua ambayo makundi ya haki yanapinga.
Mahakama ya juu pia imeamua kuwa serikali imeenda kinyume na katiba
kujiondoa kutoka ICC baada ya kushindwa kuomba ushauri wa bunge.
Jana chama tawala cha ANC, kilisema kuwa kina mpango ya kuiondoa nchi hiyo kutoka mahaka ya ICC.
Hii ni sehemu ya kampeni kubwa kutoka kwa baadhi ya nchi za kiafrika zinazodai kuwa ICC inawalenga viongozi wa bara la Afrika.
No comments:
Post a Comment