KIJANA ANUSURIKA KUFA KWA KICHAPO BAADA YA KUTAPELI KWENYE DUKA LA MPESA SHINYANGA MJINI
Kijana akijitetea
Kijana akiwa amepanda kwenye gari la polisi-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
****
Kijana mmoja ambaye jina lake
halijafahamika mara moja amenusurika kufa kutokana na kichapo kutoka kwa
wananchi wenye hasira baada ya kutapeli pesa shilingi 370,000/= katika
kibanda cha duka la Mpesa katika soko la Kambarage kata ya Kambarage
Mjini Shinyanga.
Tukio hilo limetokea leo Julai 6,2017
majira ya saa nane mchana ambapo kijana huyo alifika kwenye kibanda cha
Mpesa cha Robert Masesa kilichopo jirani na soko la Kambarage na
kutapeli kiasi hicho cha pesa.
Akisimulia kuhusu mkasa huo mmiliki wa
kibanda hicho, Masesa alisema majira ya saa tano kijana huyo alifika
kibandani hapo akitaka huduma ya kutoa pesa ,lakini alipoombwa simu yake
iangaliwe ujumbe mfupi wa maneno katika simu kama udhibitisho akawa
hana simu.
Alisema alipommbana akasema ametumia
namba ya mwingine ndipo akaagizwa amfuate ,lakini kabla hajaondoka akaja
mteja mwingine kutoa pesa ndipo akanuti yake ikasema namba yake
imefungiwa.
Masesa alieleza kuwa baada ya kupata
ujumbe huo ,ndipo akashtuka kuwa ametapeliwa na alipomuita kijana huyo
alianza kutimua mbio na baiskeli ndipo akapiga yowe na hatimaye kijana
kunaswa na na wananchi kisha kuanza kupewa kichapo.
Hata hivyo wakati wananchi hao
wakitembeza kichapo ndipo wakafika askari polisi na kumnusuru kutoka
katika kichapo hicho ambacho kiliambatana na mawe makubwa na kuokoa uhai
wake na kisha kuondoka naye kwenda kituo cha polisi.
MANYAMAJR::
No comments:
Post a Comment