Kumpata Lulu Diva unatakiwa uwe na vigezo hivi....
DIVA anayekimbiza na Ngoma ya Utamu, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefungukia
vigezo vya mwanaume anayeweza kumnasa lazima kwanza awe na ‘passion’
shauku ya maendeleo.
Unajua ipoje hii! Kama wewe mwanaume na una ndoto ya kuwa bebi wa Lulu
Diva halafu sio Smart wala Gentlemen, huna hofu ya Mungu wala kipaji cha
kudekeza, hujui kujali, una tatizo la kutokuelewa na kusikiliza basi
huwezi kumpata mrembo huyu!
Kama hutoweza kujitolea ikibidi hata maisha yako kwa ajili yake basi
nakushauri shtuka usingizini na ukemee kabisa ndoto hiyo kwani haitokaa
itimie kutokana na kukosa vigezo hivyo anavyovitaka.
No comments:
Post a Comment