HUU NDIO UJUMBEE ALIYOANDIKA PROF JAY BAADA YA KUFUNGA NDOA
Msanii
wa muziki, Professor Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph la Posta jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 na
mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo.
Cherekochereko za tukio kubwa la Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia
tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule
almaarufu Profesa Jay limetikisa Jiji La Dar baada ya kufuatiliwa na
watu wengi. Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu.
Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki
waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia
nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.
Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya
kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya
mastaa kibao wa Bongo.
“Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya
ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema
Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.
No comments:
Post a Comment