BreakingNews: Ngeleja Arudisha Mil. 40 za Escrow
Pesa hizo inadaiwa kuwa alipewa mgao yeye na baadhi ya wabunge pamoja na viongozi wengine wa serikali, dini na majaji kutoka kwa James Rugemalira wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd.
Taarifa ya kurudisha fedha hizo ameitoa leo mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema lengo la kuzirudisha ni kuhusishwa kwake na kashfa kuchotwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Ngeleja amedai kuwa fedha hizo alipewa msaada kama ilivyokuwa wabunge wengine waliogawiwa na James Rugemalira kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake la Sengerema.
No comments:
Post a Comment