WASANII:: Linex amkataa Lulu Diva
Msanii wa bongo fleva mwenye hit song
ya 'Yaongoze' Linex Sunday Mjeda amefunguka kwa kudai kwamba hamkumbuki
Lulu Diva kama mwanamuziki bali anamkumbuka kama shabiki tu.
Lulu Diva kushoto na kulia ni Linex
Linex
amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya ku
'blockiwa' na msanii mwenzake Lulu Diva kwa kile kinachodaiwa kuwa Linex
kumtukana mwanadada huyo kwenye 'comment' ya picha aliyokuwa ameweka
katika mtandao wake wa instagram.
"Inawezekana nikawa
nimem-comment kama shabiki kutokana pale nilikuwa nime-post tangazo la
biashara na ndiyo maana nikasema 'Kaka zako wanapokuwa mipangoni kwamba
wewe unatakiwa utulie...Wewe unaweza kukasirika kublokiwa na mtu ambaye
hata haumjui ?, kwanza sidhani hata kama namba yangu anayo, sijui hata
kama nimem-follow. Siyo lazima kila mtu akujue mimi mwenyewe naweza
nikapita mtaa na mtu asinijue" alisema Linex.
No comments:
Post a Comment