Trending News>>

Mdororo wa uchumi wazuia utoaji wa hati za kusafiria Brazil


Mamlaka nchini Brazil imezuia utoaji wa hati za kusafiria (pasipoti) kutokana na mgogoro wa bajeti.
Kitengo cha polisi wa uhamiaji nchini humo ambao hushughulikia utoaji wa pasipoti ndani ya siku sita za kufanya kazi, kimesema kwa sasa hakipokei maombi mapya.

Mmoja wa wanasisasa nchini Brazil amezilaumu sera za Rais Temer kwa kusababisha mgogoro wa kiuchumi.

Serikali imesema itajaribu kushughulikia suala hilo mapema iwezekanavyo, Brazil inakumbana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa hati za kusafiria waweza kuwa kikwazo wakati huu wa baridi ambapo raia wengi wa Brazil husafiri nje ya nchi.

No comments:

Powered by Blogger.