Wachezaji bongo tusiogope kwenda nje - Maguli
Mshambuliaji wa kimataifa
anayeitumikia klabu ya Dhofar SC ya nchini Oman, Elias Maguli amewataka
vijana wa Kitanzania wanaotaka kuendeleza vipaji vyao, nje ya nchi
kujaribu pale wanapopata nafasi na sio kukata tamaa.
Mshambuliaji wa kimataifa anayeitumikia klabu ya Dhofar SC ya nchini Oman, Elias Maguli.
Maguli
amesema, vijana wengi wamekuwa wakipata nafasi za kwenda katika
majaribio katika timu mbalimbali za nje ya nchi lakini wamekuwa
wakikatishwa tamaa na baadhi ya watu wanaowazunguka .
"Kwanza wanapopata nafasi
waende. Hawawezi kupata taarifa kwamba kuna ubaguzi katika hiyo nchi
unayotakiwa kwenda kabla hujafika. Fika kwanza ndio ujue matatizo
yaliyopo katika hiyo nchi, na mimi nina imani kuna wachezaji wengi
wamepata nafasi lakini labda wao wanapenda kucheza hapa nchini,” amesema Elias Maguli.
Maguli ameongeza kwa kuvitaka vilabu vya soka hapa nchini kuwaruhusu
wachezaji ili waweze kutumia nafasi wanazozipata nje ya nchi
“Kunawachezaji wengine
wameshapata nafasi lakini vilabu vimekuwa tatizo, kwani vilabu mara
nyingi huwa vinawakatalia wachezaji na hata kutaja dau kubwa na
ukiangalia sisi wachezaji wa hapa Tanzania katika viwango bado tupo
chini, hivyo tunapopata nafasi ni lazima kuzitumia ili kuweza kukuza
zaidi vipaji vyetu, ” alisisitiza Maguli.
Maguli amewataka wachezaji kutokuogopa changamoto katika soka kwani
changamoto wanazokutana nazo ndizo zinasaidia kuweza kuwakuza katika
soka.
“Unajua Tanzania kukiwa na
wachezaji wengi wa kimataifa ingekuwa ni faida kwani kila mchezaji
anapoitwa katika timu ya Taifa tungefanya vizuri zaidi ya hapa kwani
kila mchezaji anakuja na uwezo wake aliofundishwa kutoka katika klabu
yake, na pia tunajifunza vitu vingi katika maisha ya Soka, na tusiogope
changamoto kwani changamoto hata hapa nchini zipo na ndizo
zinazotusaidia kukua kisoka. Sasa kwa nini tuogope kwenda nje,
tunahitaji kuwa wengi wa kimataifa, ” amesema Maguli.
No comments:
Post a Comment