USAJILI: SportPesa yaipa kiburi Singida United, yamng’oa beki wa Simba SC
Baada ya kuhakikisha imepata udhamini mnono kutoka katika kampuni ya
michezo ya kubashiri ya SportPesa hatimaye klabu ya Singida United
inazidi kutanua misuli katika dirisha hili la usajili mara baada ya
kumsajili aliyekuwa beki wa Simba SC pamoja na Afrcan Lyon, Miraji Adam.
Mchezaji, Miraji Adam akikabidhiwa jezi ya Singida United
Timu hiyo inayonolewa na kocha Hans van der Pluijm inamkataba wa mwaka moja na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya shilingi milioni 250 huku timu hasimu za Simba pamoja na Yanga zikinufaika kwa kusaini mikataba ya donge nono na kampuni hiyo.
Klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu wa mwaka 2017 kwa ajili ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao, imefanikiwa kuwasajili wachezaji wengi wakimataifa kama vile Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa (wote kutoka Zimbabwe) na kuanza kutazamwa kama klabu itakayo leta ushindani mkubwa katika msimu mpya wa ligi hiyo.
Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu ya Singida United

No comments:
Post a Comment