Urusi Yaitimua Ndege ya NATO Iliyokuwa Ikimfukuzia Waziri wake wa Ulinzi
Ndege ya kijeshi ya Urusi, Su-27 imefanikiwa kuitimua ndege ya jeshi la NATO, F16 ambayo ilikuwa ikiifukuzia ndege aliyokuwa amepanda waziri wa Ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu
Vyombo
vya habari Urusi vimesema kuwa tukio hilo limetokea katika anga ya
kimataifa eneo la Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda
himaya ya Urusi ya Kaliningrad.
NATO baadaye ilisema ilifuatilia ndege hiyo kwa kuwa haikujitambulisha.
Kwa
mujibu wa mashirika ya habari ya Urusi ndege ya F16 ilipita karibu na
ndege ya Waziri wa Ulinzi, Shoigu, kisha ndege ya Urusi ya Su-27,
ikaingilia kati na kutoa ishara kuonyesha kuwa ilikuwa imejihami, kisha
ndege ya Nato ikaondoka.
No comments:
Post a Comment