UMOJA WA WAZAZI CCM Z’BAR WAWAASA VIONGOZI KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA AHADI ZAO WALIZOTOA
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKATIBU
wa Wilaya za Umoja wa Wazazi CCM Zanzibar wamewashauri viongozi mbali
mbali wa Chama cha Mapinduzi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi
walizotoa ndani ya taasisi hiyo ili kupunguza changamoto za kiutendaji.
Rai
hiyo imetolewa na baadhi ya Makatibu wa Wilaya Sita za Umoja huo
Zanzibar mara baada ya kukabidhiwa Komputa zilizotolelewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bi. Najma Giga ikiwa ni miongoni mwa
utekelezaji wa ahadi alizowahi kutoa wakati wa ziara zake Visiwani humo.
Katibu
wa Wazazi Wilaya ya Amani , Bi.Mwanaisha Ame Mohamed amesema
upatikanaji wa vifaa hivyo utaongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya
umoja huo kwani watakuwa na vitendendea kazi vya kisasa
vitakavyorahisisha utendaji wa kazi zao.
Aidha
Katibu huyo amewataka baadhi ya Wabunge, Wawakilishi na Madiwani ambao
bado hawajahamasika kuanza kutekeleza ahadi zao kwa umoja huo na chama
kwa ujumla kufuata nyayo za viongozi wenzao walioanza kutatua kero za
taasisi hiyo hatua kwa hatua.
“Huu
ni wakati wa viongozi mbali mbali wa Chama chetu pamoja na jumuiya zetu
kujitokeza kusaidia baadhi ya Mikoa na Wilaya zenye upungufu wa
vitendea kazi ili waweze kukamilisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.”,
alisema Katibu Mwanaisha.
Naye
Katibu wa Wazazi Wilaya ya Wete Pemba, Bi. Mariam Ali Said amemshukru
Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Zanzibar kwa kutekeleza ahadi zake kwa
vitendo na kuongeza kuwa vifaa hivyo ni chachu ya kumaliza changamoto za
kufuata huduma za uchapaji wa nyaraka za kiofisi masafa ya mbali.
Akizungumza
Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wazazi Zanzibar, Nd. Mustafa Rashid Kumwalu kwa
niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo Bi. Najma Gina mara baada ya
kukabidhi Komputa hizo ametoa wito kwa watendaji wa umoja huo kutumia
komputa hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili shughuli za kiutendaji
zifanyike kwa wakati mwafaka.
Nd.
Rashid alieleza kuwa lengo la umoja huo ni kuhakikisha watendaji wake
wanapata vitendea kazi vya kisasa vitakavyosaidia kutekeleza kwa wakati
shughuli za kiutendaji kwa lengo la kwenda sambamba na matakwa ya Katiba
ya CCM iliyofanyiwa mabadiliko miezi kadhaa iliyopita.
Aidha
alisema Komputa zilizokabidhiwa mpaka sasa ni tisa bado kumi kwa mujibu
wa idadi ya komputa zilizoahidiwa kutolewa na Naibu katibu Mkuu wa Umoja
huo, ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa kutoka ndani ya Umoja wa Wazazi
Tanzania.
Komputa
hizo zina thamani zaidi ya shilingi milioni Saba zimekabidhiwa kwa
Wilaya 6 za Umoja wa Wazazi CCM Wilaya ya Amani, Wilaya ya Mfenesini,
Wilaya ya Kati, Wilaya ya Kaskazini “B”, Wilaya ya Wete na Wilaya ya
Chake Chake Pemba.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Zanzibar , Mustafa Rashid Kumwalu
akimkabidhi Katibu wa Wazazi Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja , Bi. Salma
Shaibu, kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Bi.Najma Giga.
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Zanzibar Nd. Mustafa Rashid
Kumwala akitoa nasaha kwa Makatibu wa Wilaya Sita za Umoja huo kabla ya
kuwakabidhi komputa hizo.
Baadhi
ya Komputa zilizotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi
Zanzibar, Bi.Najma Giga kwa Wilaya Sita za umoja huo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment