Spika Job Ndugai Atoa ONYO Kwa Halima Mdee na Ester Bulaya......Atishia Kuwapa Adhabu Kali Zaidi
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni amewapa onyo wabunge Halima Mdee
pamoja na Easter Bulaya akisema kuwa wanapaswa kutambua kuwa Bunge bado
linauwezo wa kuwaita na kuwahoji na kuwapa adhabu kali zaidi ya hiyo
walionayo sasa.
Job
Ndugai amesema kuwa ameamua kutoa onyo hilo kufuatia wabunge hao
kufanya malumbano na bunge huku wengine wakitumia maneno ambayo si
mazuri hivyo amewashauri kuwa wamewavumilia kwa mengi lakini kama bado
huko waliko wanaendelea na tabia hizo wanaweza kuwaita na kuwapa adhabu
kali zaidi ya hiyo waliyonayo sasa.
"Wako
wenzetu ambao bunge hili liliwachukulia hatua za kinidhamu mbalimbali
baadhi yao wamekuwa wakijaribu kufanya malumbano na bunge na baadhi ya
kauli zao zimekuwa ni kauli ambazo si nzuri kihivyo, ningependa
kuendelea kuwashauri kwamba tumewavulimilia kwa mambo mengi lakini kama
bado huko waliko wanafikiri wanaweza kuendelea na tabia hizo huko waliko
wajue kabisa bado tunaweza kuwaita, tukawajadili kwenye bunge hili na
kuwachukulia hatua kali zaidi ya hii waliyonayo, kama mtu anataka kwenda
mahakamani unaalika watu kama mkutano wa hadhara si unaenda tu" alisisitiza Job Ndugaina kuongeza;
"Mimi
nawapa onyo tu la jumla kama ni viongozi ni vizuri kuongea lakini ongea
vitu ambavyo unataka kuongea lakini ukitaka kupambana na watu wengine
nao watataka kupambana na wewe, kwa hiyo mtapimana" alisema Job Ndugai
Spika
wa Bunge, Job Ndugai ametoa kauli hii siku moja baada ya kusifiwa na
Rais John Pombe Magufuli kuwa anakwenda vizuri kuwadhibiti watu ambao
wanaropoka bungeni na kumwambia kuwa aendelee na moto huo huo ili watu
hao wakiropoka nje ya bunge adili nao.
Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliwaadhibu wabunge Halima Mdee
na Ester Bulaya kutohudhuria vikao vyote vya Bunge linaloendelea hadi
Bunge la Bajeti 2018/2019 baada ya kuwakuta na hatia ya kudharau mamlaka
ya Spika wa Bunge.
No comments:
Post a Comment