Samatta asaini dili maalumu kwaajili ya Watanzania
Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubeligiji, Mbwana
Samatta ameingia mkataba maalumu na Benki ya DTB na pia ataendesha
kliniki ya soka kwa mamia ya vijana zoezi lililofanyika kwenye viwanja
vya Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es
Salaam.
Akizungumzia mkataba huo, Samatta alisema una lenga kuhamasisha vijana ili kuendeleza soka la Tanzania.
"Nitakuwa balozi wa DTB (Diamond Trust Bank), nikifanya kazi mbalimbali
za kijamii na masuala ya kimichezo," alisema Samatta muda mfupi baada ya
kumaliza kutoa mafunzo ya soka jana.