Ronaldo aipeleka Ureno nusu fainali kombe la mabara
Cristiano Ronaldo akishangilia kibabe baada ya kuifungia Ureno bao la 
kwanza kwa penalti dakika ya 33 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya New 
Zealand baada ya Danilo kuchewa rafu usiku wa Jumamosi Uwanja wa 
Krestovskyi mjini St Petersburg katika mchezo wa Kundi A Kombe la 
Mabara. Mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Bernardo Silva dakika ya 
37,  Andre Silva dakika ya 80 na Luis Nani dakika ya 90 na ushei. 
Matokeo hayo yanaifanya Ureno ifikishe pointi saba na kumalizana 
kileleni sawa na Mexico iliyomaliza na pointi saba pia baada ya kuifunga
 Urusi 2-1 na zote zinakwenda Nusu Fainali. Wenyeji Urusi wameungana na 
New Zealand kupanda jukwaani kitazama mechi za kumalizia michuano ya 
2017

No comments:
Post a Comment