Rasmi: Ronaldo atamka kuondoka Real Madrid
Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanamtuhumu Ronaldo, 32, kwa kutumia ulaghari kutolipa mamilioni ya ushuru.
Amekanusha tuhuma hizo.
"Anahisi kwamba amekuwa mkweli, ana sifa nzuri na alifanya kila kitu ipasavyo," ameongeza mdokezi.
Mkataba wa Ronaldo katika klabu hiyo ya Madrid una kifungu cha euro bilioni moja (£874.88m), ambacho kinafaa kufikishwa ndipo afunguliwe kutoka kwa mkataba wake.
Mdokezi aliongeza: "Amehuzunika sana na ameudhika kwa kweli."
"Hataki kukaa tena Uhispania. Kwa sasa, anataka kuondoka."
Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa £80m, alitia saini mkataba wa miaka mitano katika klabu hiyo Novemba mwaka 2016.
Mreno huyo anaweza kwenda China, lakini washauri wake wangependa aendelee kucheza soka Ulaya, pengine ahamie Paris St-Germain ya Ufaransa au arejee Ligi ya Premia.
Ronaldo, aliyewasaidia Real kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhumiwa kulaghai maafisa wa serikali ushuru wa takriban euro 14.7m (£13m; $16m) kati ya 2011 na 2014.