Mhandisi Feki akamatwa Mwanza
Wakati sakata la Vyeti fake likionekana kupungua baada ya Serikali
kuchukua hatua katika Taasisi zake na Taasisi za Umma gumzo jingine
limeibuka Mwanza leo June 16, 2017 baada ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ kumkamata mtu aliyejifanya Mhandisi wa
Jiji kisha kuomba rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU Mwanza Erenst Makale amesema mtu mmoja anayefahamika
kwa jina la James Edward ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja
amekamatwa na Taasisi hiyo kwa kujifanya Mhandisi wa Jiji kisha kuomba
rushwa ya Tsh. 200,000 kwa Mfanyabiashara.
>>>”Mtumishi huyu aliomba kwa Mfanyabiashara wa Zana za Kilimo
ambaye Zana zake aliweka kwenye eneo ambalo ni Hifadhi ya Barabara…huyu
mtu aka-take advantage (faida) akaenda kwake akijitambulisha kama
Mhandisi wa Jiji. Akamtaka aondoe Zana zake za Kilimo au ampe Shilingi
Milioni Moja. Katika kujadiliana, wakajadiliana wakashusha mpaka kwenye
Laki Mbili.
“Mwananchi huyu akawa Muungwana akaja Ofisini kwetu. Tukafanya mtego
tarehe 13, mtego huo ukafanikiwa lakini hela ilienda kupokelewa na Bwana
Godfrey Joseph Mwangonda ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkolani.
Mtu ambaye aliomba fedha ni Bwana James Edward Mwasemela ambaye ndiye
Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja.
“Baada ya kumkamata tulikuja kubaini vitu vingine vya zaida kwamba mtu
huyu James Edward Mwasemela ni sugu pamoja kwamba ni Mtumishi wa Umma
lakini ameshiriki tena kwenye makosa mengine ya utapeli na kufunguliwa
kesi mbili katika mwaka 2013 na 2016 na baadaye kesi hizo ziliondolewa…”
– Erenst Makale.