Operesheni vitabu kutinga mashuleni
Chama cha wachapishaji
binafsi nchini Tanzania (PATA) kimeiomba Serikali kuviondoa mara moja
shuleni vitabu vyote vilivyoandaliwa na kuchapishwa na Taasisi ya Elimu
Tanzania (TET) mara baada ya kubainika kutokidhi vigezo na kuwa na
mapungufu.
Akizungumza na MANYAMA.COM, Gabriel
Kitua ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho amesema vitabu hivyo
havikupitia mchakato na kufuata mwongozo wa Wizara ya elimu na ikiwa
vitaachwa mashuleni vitaleta athari kubwa katika ustawi wa elimu nchini.
Kitua amesema makosa mengi yaliyobainika
yapo kwenye vitabu vya Hisabati kidato cha tano na kidato cha
sita,historia kidato cha tatu na vitabu vyote vya kingereza kwa darasa
la tatu na kidato cha kwanza hadi nne.
Sakata la kuwepo kwa vitabu vyenye
mapungufu shuleni liliibuliwa bungeni mjini Dodoma huku tayari vikiwa
mashuleni kwa ajili ya kufundishia wanafunzi mashuleni.
No comments:
Post a Comment