Mzee Ngosha hakuwa mbunifu - Wambura
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa marehemu
Mzee Francis Kanyasu hakuwa mbunifu wa nembo ya taifa kama watu
wanavyodhania bali alikuwa mchoraji.
Wambura
amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa viti
maalumu (Chadema), Devotha Minja alilouliza juu ya serikali kushindwa
kumthaminipamoja na kumuhujumu Mzee Ngosha aliyechora nembo ya taifa na
hatimaye kufa masikini.
"Si kweli kwamba Mzee Ngosha
serikali imemuhujumu, kimsingi Mhe. Spika yapo majina mezani kama
matatu hivi yanayohusiana na ubunifu wa nembo ambayo tunaitumia, nembo
ya taifa. Kwa hiyo mpaka sasa bado haijajulikana nani hasa ambaye ni
mbunifu wa nembo hii kwa sababu mfano yupo marehemu ambaye
alishatangulia mbele za haki muda mrefu ambaye anaitwa Abdallah Farhani
wa Zanzibar yeye vielelezo tayari vishakutwa katika kumbukumbu zake
jinsi alivyokuwa akibuni nembo yetu ya taifa, nembo ya Kenya pamoja na
hata nembo ya OAU kipindi hicho alipokuwa anasoma Makerere University.
Kwa hiyo yapo majina ambayo yanadaiwa kwamba yalishiriki katika
kutengeneza nembo hii" alisema Wambura.
Pamoja na hayo Naibu Waziri amewaomba wataalamu kufuatilia kiundani kabisa juu ya suala hili ili waweze kutambua ukweli wake.
No comments:
Post a Comment