MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE YATOKANAYO NA IMANI ZA KISHIRIKINA WILAYANI MAGU.
TAREHE
13.06.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA KISABO KATA YA
BUJASHI TARAFA YA SANJO WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, NUNGHU MGETA,
MIAKA 35, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KISABO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE AITWAYE MISUNGWI NUNGHU
MIAKA 06, MTOTO WA KIUME, AMBAPO INADAIWA KUWA ALIMUUA KWA KUMZIBA
MDOMO NA PUA KWA MUDA MREFU HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUSHINDWA KUPUMUA NA
BADAE KKUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA
KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE MWENYEWE HAPO NYUMBANI
KWAKE, KWANI TAYARI ALIKUWA AMETENGANA NA MKEWE KWA MUDA MREFU.
INADAIWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUTELEKEZA MAUAJI HAYO ALIMCHUKUA
MAREHEMU KISHA KWENDA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI LILILOPO MBALI NA
NYUMBA YAKE ILI IONEKANE AMEKUFA MAJI.
ASUBUHI
WAKATI WANANCHI WANAPITA MAENEO HAYO NA KUONA MWILI WA MTOTO ALIYEPOTEZA
MAISHA UKIELEA KWENYE MAJI WALIPATA MASHAKA KISHA WALITOA TAARIFA
KWENYE KITUO CHA POLISI, ASKARI BAADA YA KUPATA TAARIFA WALIFANYA
UFATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA
MTUHUMIWA.
AIDHA
KATIKA UCHUNGUZI WA AWALI MTUHUMIWA AMEKIRI KUTEKELEZA MAUAJI HAYO DHIDI
YA MTOTO WAKE YANATOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA ILI APATE UTAJIRI.
POLISI BADO WANAENDELEA NA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA
KUHUSIANA NA MAUAJI HAYO, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA
ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA
RAI KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWAMBA HAKUNA MTU YEYETO ALIYE
JUU YA SHERIA HIVYO KILA MTU AHESHIMU NA KUULINDA UTU WA MWINGINE,
LAKINI PIA ANATAKA WANANCHI WAFANYE KAZI ZILIZO HALALI ZA KUWAPATIA
KIPATO NA KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA NA UHALIFU ILI WASIJE KUINGIA
KWENYE MATATIZO.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA