MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA SPORTPESA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ubashiri wa michezo ya
SportPesa Bw. Pavel Slavkov (kushoto), katikati ni Mkurugenzi wa
Utawala na Utekelezaji Bw. Abbas Tarimba.Viongozi hao wa SportPesa
walimtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Viongozi wa SportPesa waliofika ofisini kwake Ikulu
jijini Dar es Salaam, leo kwa lengo la kujitambulisha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa SportPesa Tanzania.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi katika mchezo kirafiki kati ya Timu
ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo
ilitwaa kombe la michuano ya Sportpesa iliyofayika hapa nchini hivi
karibuni.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali ombi hilo baada ya Kukutana
na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Kampuni inayojishughulisha na
ubashiri wa michezo ya Sports Betting nchini ambao waliongozwa na
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Tarimba Abbas Ikulu- Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepongeza mipango na mikakati mizuri
ya kampuni hiyo ya kutaka kukuza vipaji vya wanamichezo hasa kwa mpira
wa miguu kwa Tanzania Bara na Zanzibar na kusema kama malengo hayo
yatafikiwa Tanzania itakuwa bora katika mchezo wa mpira wa katika bara
la Afrika na Dunia kwa ujumla.
Makamu
wa Rais pia amewahakikishia watendaji wa kampuni hiyo kuwa milango ya
ofisi yake ipo wazi na pindi wakiwama katika jambo lolote wawasiliane na
ofisi yake ili tatizo linalowakabili liweze kutafutiwa ufumbuzi ili
lisikwamishe shughuli za kampuni hiyo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sports
Betting nchini Tarimba Abbas amemweleza Makamu wa Rais kuwa kampuni hiyo
ina malengo makubwa ya kufanya biashara hapa nchini kwa kuzingatia
sheria na kanuni za nchini.
Mkurugenzi
huyo Tarimba Abbas amesema katika mipango yao wanataka katika kipindi
cha miaka Mitatu ijayo kampuni yao iwe ni moja ya kampuni bora nchini
katika ulipaji wa kodi kwa Serikali kama wanavyofanya kwa sasa katika
Serikali ya Kenya.
Amesema
mipango na mikakati waliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha wanainua vipaji
vya wanamichezo nchini kwa sababu Tanzania Bara na Zanzibar kuna vipaji
vingi vya wachezaji wa mpira wa miguu ambavyo haviendelezwi ipasavyo.
Watendaji
wa Kampuni hiyo pia wamemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ombi lao na kuwa Mgeni
rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini
Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo ambao unatarajiwa
kufanyika tarehe 13 Julai mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sports Betting nchini Tarimba
Abbas amesema moja ya lengo la kuileta Timu ya Everton nchini ni pamoja
na mambo mengine ni kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii nchini
kupitia mchezo huo ambao unatarajiwa kuangaliwa na maelfu ya watazamaji
Duniani kote.
Mkurugenzi
huyo pia amemweleza Makamu wa Rais kuwa tayari wameshawasiliana na
mamlaka inayohusika na masuala ya utalii nchini ili iweze kutumia fursa
hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini kama hatua
ya kuongeza idadi ya watalii watakaokuja kutembelea vivutio nchini na
kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta hiyo.