MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017 JIJI LA MBEYA
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bi.Susan Mlawi akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa
viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya alipofanya ziara ofisini hapo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma 2017.
Mkurugenzi
Idara ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky
Kiliba,akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za OPRAS zinazopima
utendaji kazi wa mtumishi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bw. Musa Mapunda (wa pili kutoka kushoto)
akieleza majukumu ya jiji hilo wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji
hilo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (kulia) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Kaimu
Katibu Tawala wa Jiji la Mbeya Bw.Nyasembwa Sivangu akisoma taarifa ya
Jiji la Mbeya wakati wa kikao kati ya viongozi wa Jiji hilo na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Bi.Susan Mlawi (wa pili kutoka kulia) ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia ni Mkurugenzi Idara
ya Uchambuzi na Ushauri kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw.Micky Kiliba.
Mmoja
wa watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya akiuliza swali wakati wa
ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora Bi.
Susan Mlawi (hayupo pichani) jijini hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Viongozi
wa Halmashauri ya Jiji la mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais,Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Bi.Susan Mlawi (hayupo
pichani) alipofanya ziara jijini hapo mapema leo lengo ikiwa ni
kusikiliza changamoto wanazokutana nazo waajiri katika Utumishi wa Umma
na kuzipatia ufumbuzi. Ziara hiyo ni moja ya Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma 2017.