Jaji Mwingine wa Mahakama Kuu AJIUZULU......Rais Magufuli Aridhia
Aliyekuwa
Jaji wa Mahakama Kuu Mhe. Mwendwa Judith Malecela amejiuzulu wadhifa
wake huo kuanzia leo baada ya Rais Magufuli kukubaliana na ombi la jaji
huyo aliyetaka kujiuzulu wadhifa wake.
Katika
taarifa iliyotolewa na Ikulu leo imedai kuwa Rais Magufuli amekubaliana
na ombi la Jaji huyo hivyo kuanzia leo tarehe 20 Juni, 2017 Judith
Malecela hatakuwa tena Jaji wa Mahakama Kuu.
No comments:
Post a Comment