Trending News>>

Hatimaye mchezaji wa Yanga Mrwanda Haruna Niyonzima atua simba



Taarifa zinaeleza kuwa Mchezaji wa Soka  Kimataifa kutoka Rwanda  Haruna Niyonzima amaliza muda wa Kibarua chake ndani ya Klabu ya Yanga na kutimkia kwenye Klabu ya Soka ya Msimbazi Simba.

chanzo chetu cha habari kimedai kuwa hivi karibuni itadhihirika Niyonzima kuwa atakuwa ni mchezaji wa Klabu ya Simba.

Awali Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.

Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.

Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla

No comments:

Powered by Blogger.