Trending News>>

Habari kubwa mbili zilizoripotiwa kwenye Taarifa ya Habari usiku huu....

Mix


Usiku wa June 29, 2017 zimeripotiwa taarifa mbalimbali kwenye Televisheni za Tanzania ambapo kama ulikosa hii ni time yako kuzisoma hizi kupitia MANYAMAJR  ambapo miongoni mwa habari nyingi hizi hapa ni kubwa mbili zilizosomwa Channel 10 na TBC1.
Habari ya Channel 10 – Mahakama yawakubali mawakili wapya 248
Mahakama Kuu ya Tanzania imewakubali Mawakili 248 ambao watakwenda kufanya kazi katika Mahakama mbalimbali nchini kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata msaada wa kisheria na kuepuka rushwa.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amesema kuongezeka kwa idadi ya Mawakili kutasaidia nchi kufikia malengo yake ikiwemo kutafsiri mikataba mbalimbali na kuwafikishia msaada wa kisheria wananchi walio pembezoni.
>>>“Huo weledi waendele kuwa nao iliwaweze kuwatumikia wananchi, jambo linguine ni swala la madili na rushwa ni swala lisilo la kufumbiwa macho linaongelewa.” Prof. Ibrahim Juma.
“Kwa idadi ya walioingia leo 248, kutakuwa na Mawakili 6,329 ambao ni Mawakili binafsi. Kwa hiyo, kuna uwezokano mkubwa wa kuongezeka kwa huduma za kiwakili na huduma za kisheria kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Mawakili. Ni jambo jema” – Tundu Lissu (Rais wa Chama cha Wanasheria).

Habari ya TBC1 – Serikali kuhusu mtandao wa Dawa za Kulevya
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuendelea kupambana kutokomeza na kuvunja mitandao ya waingizaji, wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya nchini.
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Dawa za Kulevya yaliyofanyika kitaifa Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka Wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.
>>>“Kila Mtanzania aumie kwa hili na kila mmoja apate uchungu kwa hili kwamba ni jambo lisilokubalika ndani nchi yetu na kwa maana hiyo lazima tuape mbele yenu tutapambana na kila mmoja anayetumia, anayesambaza, anayekula dawa za kulevya na wala usifanye mzaha na usijaribu.” – Kassim Majaliwa.

No comments:

Powered by Blogger.