WANAFUNZI WATATU WAFA MAJI GEITA
Baadhi ya viongozi wa kiserikali na wakidini pamoja na wananchi wakiwa kwenye ibada ya mazishi ya watoto watatu ambao wamekufa maji . |
Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita waki shuhudia miili ya marehemu . |
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akitoa pole kwa wafiwa wa tukio la watoto watatu ambao wamekufa kwenye maji ziwa Viktoria. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akitoa pole kwa wafiwa wa tukio la watoto watatu ambao wamekufa kwenye maji ziwa Viktoria. |
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo la tukio. |
Usafiri wa Boti ambao wamekuwa wakitunmia wanakijiji wa Kisiwa cha Lulegea ambacho ndio kiliwaacha wanafunzi kabla ya tukio kutokea. |
Baadhi ya abilia wakishuka kwenye kivuko hicho. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Lulegea. |
Baadhi ya watoto ambao wamenusurika wakati wa dhoruba ambalo lilitokea |
MATUKIO YOTE YA PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE
Kufuatia tukio la wanafunzi 24 kuzama maji ziwa viktoria na wengine watatu kupoteza maisha wakati wakitokea masomoni Kijiji cha Butwa na wakielekea Kitongoji cha Lulegea Kata ya Izumacheli Wilaya na Mkoa wa Geita,Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameagiza halmashauri ya Wilaya pamoja na wananchi wa kijiji hicho kuwa na ushirikiano ili kujenga shule kwenye kisiwa hicho.
Hayo
ameyasema wakati alipokuwa akitoa pole kwa wafiwa na jamii ambayo ipo kwenye
kisiwa hicho kutokana na tukio la kufariki kwa wanafunzi watatu wa shule ya
msingi Butwa wakati wakitokea shule kurudi Nyumbani.
Mh,Kyunga
amesema kuwa ili kuwasaidia wananchi wa Kitongoji cha Lulegea hawana budi
kujenga shule na kwamba wakati utakapokuwa umetulia wa mvua ni vyema kwa
wananchi kujumuika kwa pamoja na kushirikiana ili waweze kujenga shule ambayo
itawasaidia wananfunzi.
“Mimi pia nimesikitishwa sana na msiba huu wa
wanafunzi hawa lakini ni muhimu kutafuta suluhisho la matatizo haya kwa wanafunzi na suluhisho ni serikali na nyie wananchi
kujitokeza kuchangia nguvu ili tuweze kujenga shule kwenye eneo hili ili
matatizo ya namna hii yasiweze kujirudia tena siku nyingine”Alisema Kyunga.
Tululaza
Kurulahenda ambaye alikuwa amewabeba wanafunzi hao kwenye Mtumbwi ambao ulizama
ameelezea kuwa chanzo ambacho kilisababisha ajali hiyo ni kutokana na watoto kutokutulia wakati akiendesha
mtumbwi pamoja na hali kutokuwa shwari
ya ziwani.
“Muda
ulikwenda sana na boti ambayo huwa inawabeba wanafunzi ilikuwa
imekwisharudi moja kati ya mama ambaye mtoto
wake amefariki akaniomba niwafuate na mtumbwi namimi sikubisha kwakuwa walikuwa
ni watoto ikabidi niwafuate kwa bahati mbaya wakati ninarudi nikiwa nimekaribia
kufika upande wa pili hali iliharibika na kukawepo na upepo hali ambayo
ilipelekea wanafunzi kuanza kupiga kelele na kuruka lakini hata hivyo mimi
pamoja na mwanafunzi ambaye anaitwa Tisekwa tulianza juhudi za kuwaokoa wengine
ndipo na tukawa tumefanikisha baada ya
baadhi ya wavuvi wenzangu kuja kutusaidia na tulipowaokoa tukagundua kuwa
watatu hawaonekani ndipo tukaanza mchakato wa kuwatafuta baada ya juhudi majira
ya saa moja tukaupata mwili wa mwanafunzi mmoja akiwa amefariki wengine
tumewapata asubuhi”Alisema huku akiwa na masikitiko Tululaza.
Aidha
Tisekwa Gamungu ambaye ni mtoto aliyewaokoa wenzake amesema kuwa walikuwa
wakitoka shuleni wakati wakiwa njiani wakirudi waliona kama kimbunga kimetokea hali
ambayo ilipelekea wengi wao kulia huku wakiombwa kurudishwa kule ambako
wametokea.
Wanafunzi ambao wamepoteza maisha kwenye tukio hilo ni Kumbuka Bruno Thomas (13) ni mwanafunzi wa darasa la tano ,Anastazia Christopha (12)darasa la tatu na Sophia Muungano (11)darasa la pili .